Sunday, November 15, 2009

Tundaman akimbia Timbwili Timbwili

Tundaman akimbia Timbwili Timbwili
...
Msanii wa kundi la muziki la Tip Top Connection Khaleed Ramadhan a.k.a Tundaman hivi majuzi alijikuta akichezea kichapo toka kwa mmoja wa wadada aliyekuwepo kwenye ukumbi wa Travertine Magomeni kumshushia kisago.
Akiitonya Dar411 shuhuda wetu aliyekuwepo kwenye ‘Timbwili’ hilo alisema ilianza kama utani baada ya Star huyo toka pande zile za Manzese kukuta bonge la ugomvi kati ya wadada wawili waliokuwepo ukumbini hapo na kuingilia kati kutaka kusawazisha mambo na ndipo mmoja wa wadada hao alipofanikiwa kuchoropoka, sasa kazi ikabaki kwa yule dada aliyebaki ambaye alianza kumlaumu Tundaman kwa kitendo chake cha kuingilia ugomvi usiomhusu.
Baada ya kuona haitoshi kulalamika akaanza kumrushia mawe Tundaman ambaye alipoona timbwili hilo haliwezi aliamua kula kona.

No comments:

Post a Comment